Shule nyingine ya wavulana yateketea kwa moto Kenya,Ruto ataka uchunguzi ufanyike haraka

Kisa kingine cha moto shuleni kiliripotiwa katika Shule ya sekondary ya Wavulana ya Isiolo Boys siku ya Jumanne jioni.

Katika taarifa, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya lilisema timu ya kukabiliana na tukio hilo ilikuwa imetumwa.

Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

Haya yanajiri wakati kuna milipuko ya matukio ya moto shuleni kote nchini.

Kisa cha moto katika Shule ya Upili ya Wavulana ya Isiolo kinakuja siku tatu tu baada ya moto mwingine kuripotiwa katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Isiolo.

Kisa hicho pia kinajiri siku chache baada ya moto katika shule ya Hillside Endarasha huko Nyeri kuwaua wanafunzi 21.

Wachunguzi bado wanafuatilia kisa hicho ili kujua chanzo cha moto huo.

Siku ya Jumatatu, Rais William Ruto alifanya mkutano na viongozi kutoka wizara ya Mambo ya Ndani na Elimu.

Ruto aliagiza kukamilika kwa haraka kwa uchunguzi kuhusu mkasa wa moto wa shule ya Hillside Endarasha Academy

 

The post Shule nyingine ya wavulana yateketea kwa moto Kenya,Ruto ataka uchunguzi ufanyike haraka first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/cG1Y4xa
via IFTTT

Post a Comment

0 Comments