Wachezaji wa Yanga Mudathir Yahya, Bacca, Job, Mwamnyeto, Nickson Kibabage, na Clement Mzize wameondoka saa tisa alfajiri Ivory Coast ambayo ni sawa na saa kumi na mbili asubuhi kuelekea Abidjan, Abidjan wataondoka saa tano ya Ivory Coast ambayo ni sawa na saa nane nyumbani Tanzania kuelekea nchini Ethiopia.
Kikosi kilichosalia kinaondoka Abidjan saa mbili usiku kwa hapa Ivory Coast na ni sawa na saa tano nyumbani Tanzania na kitawasili Dar Es Salaam kesho September 12, saa nane mchana.
Wachezaji Novatus Dismas na Cyprian Kachwele wanaondokea huko huko Ivory Coast, Novatus Dismas Miroshi anaenda Uturuki na Cyprian Kachwele anaenda Canada wote wanatumia shirika la ndege la Turkish Airlines.
Wachezaji wa Simba Sports Club Ally Salim, Mohammed Hussein, Edwin Balua na Moussa Camara wameondoka jana hapa Yamoussoukro, wameondoka kwenda Libya leo saa tisa alfajiri ambayo ni sawa na saa kumi na mbili asubuhi Tanzania.
Timu hizo zinakabiriwa na michezo ya Kimataifa, Wikiendi hii, ambapo Yanga watacheza Ligi ya Mabingwa Afrika Septemba 14 Jumamosi, huku Simba wakicheza Kombe la Shirikisho Afrika siku ya Jumapili Seotemba 15
The post TAARIFA MPYA KUHUSU SIMBA NA YANGA…MUDA HUU appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/rJPAfHw
via IFTTT
0 Comments