
Athari ya shinikizo kubwa kwa mifumo mibovu ya majitaka. Picha|Labaan Shabaan[/caption] Kulingana na wakazi wa mitaa hii, serikali imewasahau kwa muda mrefu. “Tangu Kenya ipate uhuru, hatujawahi kuwa na mfumo wa majitaka. Sasa tuna kitu cha kufurahia kuhusu ugatuzi. Watoto wetu wamekuwa wakiambukizwa magonjwa,” akalalamika Beatrice Adisa, mkazi wa Flamingo ambapo kuna wakazi 1,000. Bw James Kiarie, mkazi wa Kivumbini anasema: “Nimeishi hapa kwa zaidi ya miaka 30 ambapo milipuko ya magonjwa imekuwa tukio la kawaida kwa sababu ya uchafu. Mfumo wa majitaka wa kisasa ni afueni kwetu.” Diwani wa Kivumbini Neto Sakwa anakatilia mkazo matarajio ya wakazi. “Mradi huu utaimarisha miundomsingi ya maji na usafi katika Jiji la Nakuru. Wakazi wameteseka kwa miaka mingi kutokana na msururu wa maradhi,” akasema Bw Sakwa. Wakazi wa mtaa mkongwe wa Paul Machanga pia wana matarajio makubwa. Bw Mohammed Ali ameishi hapa kwa muda mrefu na anaelewa historia yake. “Mtaa huu una zaidi ya nyumba 200 ambazo zinasimamiwa na serikali ya kaunti. Wakazi watanufaika pakubwa,” Bw Ali aliambia Taifa Leo. Gavana wa Nakuru Susan Kihika amesifu mradi huu akisema utadhibiti hali ya kuvuja kwa mifereji ya majitaka. “Nakuru sasa ni jiji na ni lazima iwe kipaumbele ukizingatia kuwa na maji safi na mfumo mzuri wa majitaka,” Bi Kihika alisema. Gavana Kihika alifichua kuwa mradi huu ni Sh5.6 bilioni na unafadhiliwa na Benki ya Germany Development Bank (KfW). Kulingana na Bi Kihika, gatuzi hili litashirikiana na washikadau wengine kuimarisha mifumo ya maji katika miji mingine pamoja na Molo na Gilgil. [caption id="attachment_164444" align="alignnone" width="2560"]
Majitaka yatapakaa baada ya mifereji kuvuja. Picha|Labaan Shabaan[/caption] Kulingana na takwimu za Kaunti ya Nakuru, familia zinazoishi Nakuru hutoa takriban lita 300 za majitaka kwa siku. Ni wakazi wa mitaa ya hadhi ya juu ambao wananufaika na muunganisho wa mfumo wa majitaka. Mitaa hiyo inajumuisha Milimami, Langa Langa, London, eneo la katikati ya jiji (CBD), Racecourse na Freehold. IMETAFSIRIWA NA LABAAN SHABAANfrom Taifa Leo https://ift.tt/IRKZ7Qw
via IFTTT
Tags
TRENDING NEWS