
Kwa mujibu wa polisi, tukio hilo lilitokea karibu na vituo vya kupigia kura vya Chelemei na Kiribwet katika wadi ya Kapsasian, ambapo waliojeruhiwa walikimbizwa katika hospitali mbalimbali kupatiwa matibabu.
Tukio hilo lilitokea wakati wapiga kura 44,457 wa eneo bunge la Emurua Dikirr, Kaunti ya Narok, walipokuwa wakiendelea kupiga kura kumchagua mrithi wa aliyekuwa Mbunge wa awamu tatu Johana Ngeno.
Tume ya IEBC iliwaidhinisha wagombeaji David Kipsang Keter (UDA), Desma Cherono (PNU), Vincent Rotich (DCP), Gideon Koech (NVP) na Kenneth Kiprono (RLP).
Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Narok Patrick Lobolia alithibitisha vurugu kati ya wafuasi wa UDA na DCP, huku wagombea wakitoa wito wa utulivu na kuimarishwa kwa usalama kuzuia kuongezeka kwa mvutano.
from Taifa Leo https://ift.tt/bS8gGAM
via IFTTT