
Aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga akishiriki densi na vijana wa Gen Z wakati wa hafla ya The People Dialogue Festival (PDF), Machi 6, 2025. Picha|Francis Nderitu[/caption] Bw Maraga amejizolea sifa kedekede kama mpiganiaji wa haki na masuala ya uongozi. Hasa amekuwa akipigania mageuzi ya kitaasisi kusaidia kupambana na ufisadi. Alipokuwa jaji mkuu, aliwaongoza majaji wa mahakama hiyo kufuta uchaguzi mkuu wa Agosti 2017 kutokana na udanganyifu na wizi wa kura. Hii ilikuwa mara ya kwanza ambapo mahakama ilifuta uchaguzi wa urais barani Afrika na kuashiria uhuru wa korti tangu uhuru upatikane. Mnamo 2020, Bw Maraga alimshauri aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta kuvunja bunge kwa kukosa kutekeleza sheria ya thuluthi mbili jinsi inavyotakikana kwenye katiba. Pia alishutumu juhudi zinazoendelea za kuwaondoa majaji wa mahakama ya juu wakiongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome, akisema zinalenga kutimiza tu maslahi ya kisiasa. “Tatizo ni kuwa tuna watu ambao wanaibuka na madai yasiyo kweli. Soma maombi ya kuwaondoa majaji hao jinsi yalivyowasilisha na yaliyomo kisha uone mahali ambapo tatizo linatokea,” akasema. “Iwapo masuala yaliyoibuliwa kwenye maombi yangewasilishwa kisheria kwenye idara husika, basi hili suala lingepata utatuzi. Ni suala la ukosefu wa uaminifu na kuwasaidia wengine kutimiza ajenda zao za kisiasa,” akasema. Alisema kuwa wakati ambapo alikuwa jaji mkuu, masuala hayo yalishughulikiwa na Tume ya Huduma za Mahakama (JSC). “Kama kuna madai ya ufisadi, leta ushahidi. Huwezi kusema tu jaji mkuu anastahili kuondolewa afisini kwa sababu alitoa uamuzi ambao haukubaliani nao,” akasema. “Watu walikuwa wakiniandikia kuwa wanataka jaji aondolewe afisini kwa sababu ametoa uamuzi usiowapendeza. Nilikuwa nawaambia waende katika mahakama ya rufaa,” akasema. Majaji wa mahakama ya juu wanakodolewa macho na maombi ya kuondolewa afisini baada ya kutoa uamuzi wa kumzima wakili Ahmednasir Abdullahi kuwakilisha wateja wake kwenye mahakama hiyo. Hii ilitokana na hatua ya Bw Abdullahi kuwakashifu Bi Koome na wenzake kwenye mitandao kuhusu jinsi ambavyo walivyokuwa wakiendesha idara ya mahakama. Maombi hayo yamewasilishwa na mawakili Nelson Havi na Christopher Rosana.from Taifa Leo https://ift.tt/gwFqS4E
via IFTTT
Tags
TRENDING NEWS