
Kutoka kushoto, mwenyekiti wa kitaifa Baraza Kuu la Waislamu Nchini (Supkem) kwenye kikao na wanahabari jijini Nairobi mnamo Ijumaa, Machi 28, 2025 akitoa taarifa kuhusu hali ya Stephen Munyakho kuachiliwa huru. PICHA|CHARLES WASONGA[/caption] Wakati wa mkutano huo Katibu Mkuu wa MWL Dkt Mohamed AbdulKarim Alissa, alijulishwa kuhusu kesi ya Munyakho na kuombwa aingilie kati. Kulingana na Ole Naado, kwa kuwa Munyakho na marehemu walikuwa marafiki kabla ya wao kupigana, suala hilo lilichukuliwa kwa uzito katika baraza la MWL. Mamake Munyakho, Dorothy Kweyu, aliongea na wanahabari kupitia mtandao wa WhatsApp na kuthibitisha kuwa Sh129.5 milioni zilizotolewa na baraza la MWL zimelipwa familia ya mhasiriwa. “Mimi kama mamake Stevo nathibitisha kuwa Baraza la Waislamu Ulimwenguni limelipa pesa za fidia ya damu kwa familia ya marehemu aliyekufa kwa bahati mbaya baada ya kupigana na mwanangu wakiwa kazini Saudi Arabia. Sasa tunasubiri mahakama kuandaa kibali cha kuachiliwa huru kwa Stevo kutoka gerezani ili arejee nyumba,” akaeleza. Mama Kweyu, ambaye ni mwanahabari tajika, alitoa shukrani kubwa kwa baraza la MWL na wahisani wote waliojitokeza kutoa michango ya kusaidia kulipa fidia hiyo. “Ama kwa hakika natoa shukrani kubwa zaidi kwa usaidizi huo. Tulikuwa tumefaulu kuchanga Sh20 milioni pekee ambazo zilikuwa kiasi kidogo zaidi zikilinganishwa na Sh129.5 milioni zilizotakikana. Aidha, nashukuru vyombo vya habari kwa kusaidia kuendesha michango na kuangazia madhila ya mtoto wangu Stevo,” akaeleza. Habari kuhusu kulipwa kwa fidia hiyo ilifichuliwa kwa mara ya kwanza na Katibu Mkuu wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) Hassan Omar Jumanne wakati wa Iftar iliyoandaliwa katika Ikulu ya Nairobi.from Taifa Leo https://ift.tt/yHK5YOk
via IFTTT
Tags
TRENDING NEWS