
Mmiliki wa nyumba karibu na Mto Nairobi Issa Hassan. Picha|Labaan Shabaan[/caption] “Mimi siko tayari kuhama na endapo nitaondoka eneo hili, serikali haiwezi kunilipa hata nikiwa na hatimiliki ya ardhi,” akateta Bi Minayo. Ukanda wa mita 60 umetengwa kutoka mtoni kuwa eneo la chemchemi katika mita 30 na sehemu iliyobaki kustawishwa kwa miradi ya serikali. Maeneo yatakayoathiriwa ni kutoka Naivasha Road hadi Ruai, kipaumbele kikiwa ujenzi wa nyumba za bei nafuu zinazoendelezwa na serikali ya Kenya Kwanza. Mipango hii ni kulingana na notisi ya tarehe 6 Machi 2025 iliyotolewa na Waziri wa Mazingira Kaunti ya Nairobi Patrick Mbogo kutaka wananchi watoe maoni yao kwa kipindi cha majuma mawili kabla ya kutekelezwa kwa miradi. Mkutano uliosimamiwa na washikadau wa serikali Kawangware kukusanya maoni ya wananchi ulivurugika juma lililopita kwa sababu ya kukosekana kwa mwafaka. Wakazi waliozungumza na Taifa Leo walionyeshwa mafadhaiko yao kuhusu miradi ya serikali. “Makaburi ya babu zetu yako hapa na hatufai kuenda mbali nayo. Naomba serikali iangalie tena mpango huu na kusikiza malalamishi yetu,” akasema Ali Macharia mwenye umri wa miaka 74. [caption id="attachment_170886" align="alignnone" width="1920"]
Mzee mwenye umri wa miaka 74 Ali Macharia. Aomba Rais William Ruto asitishe mpango wa kuwahamisha. Picha|Labaan Shabaan[/caption] Naye mkazi mwenzake Issa Macharia akaongeza: “Sisi hatutasonga hata inchi moja na hawafai kukaribia mashamba yetu na kukiuka haki zetu.” Serikali ya Kaunti ya Nairobi inasema hatua hii imechochewa na ombi kutoka Wizara ya Ardhi, Ujenzi, Makazi na Ustawishaji. Serikali kuu inaendesha mpango wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu katika kingo za Nairobi River pamoja na uboreshaji wa mazingira ya mito kudhibiti wa mafuriko. [caption id="attachment_170887" align="alignnone" width="1920"]
Mto Nairobi eneo la Riruta Muslim Village, Kawangware. Picha|Labaan Shabaan[/caption]from Taifa Leo https://ift.tt/hJmfHcn
via IFTTT
Tags
TRENDING NEWS