Changamoto za uundaji IEBC mpya zatia doa kura ya 2027

MIPANGO na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2022 huenda yataathirika kutokana na kutokamilika kwa mchakato wa kuteua Mwenyekiti na makamshina wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Nchini (IEBC). Makato ya bajeti, madeni mengi, kucheleweshwa kwa kuwekwa kwa mipaka mipya na pingamizi za upinzani ni kati ya vikwazo ambavyo vinaandama IEBC inayoongozwa na Erastus Ethekon hata kabla haijaanza kazi. Majina ya mwenyekiti na makamishina wa IEBC yalichapishwa na Rais William Ruto kwenye gazeti rasmi la serikali mnamo Juni 10, 2025 lakini uteuzi wao umekwamishwa na korti. Mnamo Mei Mahakama Kuu ilitoa amri ya muda ya kuzuia kuchapishwa kwa majina na kuapishwa kwa makamishina wapya wa IEBC. Kesi iliyowasilishwa ilisema Rais hakufuata katiba na baadhi ya walioishia kuteuliwa hawastahili kupitia kigezo cha maadili. Pia walisema uteuzi huo ulifanyika bila upinzani kuulizwa, hali ambayo inakiuka katiba, sheria ya uchaguzi na mapendekezo ya Ripoti ya Jopo la Maridhiano maarufu kama NADCO. Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kesi hiyo mnamo Julai 8 2028. [caption id="attachment_170327" align="alignnone" width="500"] Masanduku ya kura ya IEBC. PICHA|MAKTABA[/caption] Mkwamo huu wote umezua maswali iwapo uchaguzi wa 2027 utakuwa wa haki wakati ambapo vijana nao wamekuwa wakipambania mabadiliko. Mshauri wa Rais William Ruto kuhusu masuala ya uchumi Moses Kuria amesema siku 39 zijazo Wakenya wataanza kuhesabu miaka miwili kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi mkuu. Bw Kuria alisema Tume ya Kriegler ambayo ilichunguza na kutoa mapendekezo yake baada ya uchaguzi mkuu wa 2027, ilisema kuwa uchaguzi mkuu hauwezi kuwa huru iwapo tume haitakuwa imeundwa miaka miwili kabla ya kura hiyo. “Ukitathmini mchakato wa korti suala hili huenda likaishia hadi Mahakama ya Juu hadi Septemba 2027. Kwa hivyo, utawala wa sasa utaendelea kuwa mamlakani kama uchaguzi haujaandaliwa,” akasema Bw Kuria. Upinzani nao hauonekani kulegea katika shinikizo zake ikisema kuna njama ya kuiba kura mnamo 2027 kwa sababu walioteuliwa ni washirika wa Rais Ruto na chama tawala. “Serikali haiwezi kujishauri pekee bali lazima ishauriane na upinzani. Kuwa na tume ambayo Wakenya hawana imani nayo ni kama kunyoosha njia ya kuiba kura ambayo Wakenya hawatakubali,” ikasema taarifa ya upinzani mnamo Aprili. Ingawa hivyo, hata makamishina wa IEBC wakiapishwa, itabidi pia wajikune kichwa kuhusu ukosefu wa fedha za kuandaa chaguzi ndogo. Afisa Mkuu Mtendaji wa IEBC Marjan Hussein Marjan alisema kuwa hatima ya chaguzi ndogo katika maeneobunge yaliyowazi na viti vya udiwani haijulikani kutokana na ukosefu wa fedha. Bw Marjan alisema kuwa chaguzi hizo zinastahili kugharimu Sh215.84 milioni ambazo tume hiyo haijapewa.

from Taifa Leo https://ift.tt/5BaYjFI
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post