Jumatano Agosti 28 2024
Atamrithi Dk Matshidiso Rebecca Moeti wa Botswana, ambaye mihula yake miwili ya miaka mitano inamalizika kwenye kikao hicho.
Dk Faustine Ndugulile wa Tanzania alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika Jumanne katika kikao cha Kamati ya WHO Kanda ya Afrika kinachoendelea Brazzaville, Kongo.
Alipata kura 25 kati ya 46 na kuwashinda wagombea kutoka Rwanda, Niger na Senegal. Aliungwa mkono na nchi 25 za Afrika, ikiwa ni pamoja na Kenya.
Aliyekuwa naibu waziri wa Afya nchini Tanzania, Dk Ndugulile atamrithi Dk Matshidiso Rebecca Moeti wa Botswana, ambaye mihula yake miwili ya miaka mitano inamalizika kwenye kikao hicho.
Dk Ndugulile, daktari bingwa wa microbiology, ana uzoefu mkubwa katika afya ya umma.
Katika kampeni zake za kuwania nafasi hiyo, alisema vipaumbele vyake ni pamoja na kubadilisha mifumo ya afya ya Afrika ili kufikia huduma ya afya kwa wote, kuboresha afya ya mama na mtoto na kuimarisha usalama wa afya, ubunifu na utafiti. "Kugombea kwangu kunawakilisha juhudi za pamoja za kubadilisha hali ya afya ya Afrika.
Kwa kutanguliza huduma ya afya kwa wote, afya ya mama na mtoto,” aliambia The EastAfrican mapema.
Pia alisema atalenga kuimarisha ushirikiano kati ya serikali za Afrika na taasisi za afya. Dk Ndugulile alisisitiza haja ya kuboresha fahirisi ya huduma kwa afya kwa wote, ambayo imesalia chini ya asilimia 50 katika nchi nyingi za Afrika.
Dk Ndugulile kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Kigamboni jijini Dar es Salaam na anahudumu kama Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya na VVU/UKIMWI Tanzania, Umoja wa Mabunge (IPU) na NEAPACOH.
0 Comments