
Bi Orwoba ambaye alikuwa Seneta Maalum kabla ya UDA kumvua wadhifa huo mwezi Mei 'kwa kushirikiana na mrengo hasimu'.Picha|Charles Wasonga[/caption] Katika uamuzi wake, Hakimu Ngotho alibaini kuwa jumbe ambazo Bi Orwoba aliweka katika mitandao ya kijamii alikidai Bw Nyegenye alimdhulumu zilimharibia jina, “kusababishia msongo wa kiakili na kumwaibisha karani huyo wa Seneti.” Aidha, hakimu huyo alimwagiza Orwoba kumwomba masamaha Bw Nyegenye hadharani ndani ya muda wa siku 30 la sivyo alipe Sh1 milioni zaidi. Isitoshe, Hakimu Ngotho alimzima Bi Orwoba au washirika wake kuchapisha taarifa zozote za kumharibia jina karani huyo wa Seneti. Mnamo Mei 19, 205 chama cha United Democratic Alliance (UDA), kilichomteua kama Seneta, kilimvua uanachama. Chama hicho kilisema kilimpata Orwoba na hatia ya kuvunja kanuni na sheria zake kwa kushirikiana na mrengo hasimu wa kisiasa. Bi Orwoba ni miongoni mwa wanasiasa kutoka jamii ya Kisii ambao mnamo Aprili 24, 2025 walimlaki aliyekuwa Waziri wa Usalama Fred Matiang’i aliporejea nchini kutoka Amerika.
from Taifa Leo https://ift.tt/rzYwuNL
via IFTTT
Tags
TRENDING NEWS