Mshangao pasta akimbaka binti ya mwenyeji wake Kisumu

MKUTANO wa viongozi wa kidini mjini Kisumu uliolenga kusherehekea imani yao na kupalilia ushirikiano ulikumbwa na maovu baada ya bintiye pasta mwenyeji wao kubakwa na mmoja wa waalikwa. Kisa hicho kilitokea Agosti 21, 2025 katika jumba la malazi la Dignitaries Guest House mtaani Manyatta, biashara inayomilikiwa na pasta mwenyeji na mkewe. Kundi la mapasta walikuwa wakikutana katika jumba hilo kwa shughuli iliyosemekana kulenga kuimarisha umoja ndani ya kanisa lao. Kulingana na polisi, mwanamke mwenye umri wa miaka 24, ambaye amepooza sehemu fulani ya mwili, alikuwa ameagizwa na msimamizi wake kuwapelekea maji moto katika vyumba walikokuwa wakikaa mapasta hao wageni. Mwendo wa adhuhuri, mwanamke huyo aliingia ndani ya mojawapo ya vyumba, ambako pasta huyo, mmoja wa wageni, alikuwa akikaa. “Alikuwa akimwaga maji ndani ya karai ndipo mshukiwa akamkamata kwa nguvu na kumrusha kitandani, kisha akambaka,” ikasema ripoti ya polisi kuhusu tukio, OB Nambari 51/12/09/2025. Kulingana na taarifa ambayo mama huyo aliandikisha kwa polisi, alipoingia ndani ya chumba hicho, mshukiwa alimkamata na kumbaka. “Alipiga mayowe lakini alijilazimisha kwake. Nilifika hapo haraka na kumpata juu ya msichana huyo,” akaeleza mwenzake kwa jina Charity, ambaye aliwaambia wapelelezi alivutiwa na kilio cha mwathiriwa.


from Taifa Leo https://ift.tt/dtn16oR
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post