
MAAFISA wa afya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wameanza kutumia data ya simu za mkononi kufuatilia mienendo ya watu na kutambua maeneo ambayo Ebola inaweza kuenea.
Hii ni kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Teknolojia hiyo, ambayo haijawahi kutumika katika kukabiliana na mlipuko wa Ebola, huchanganua taarifa mbalimbali ya mawasiliano ya watu.
Hivyo, wataalamu wanaweza kukadiria maeneo ambayo watu husafiri na kutambua maeneo yaliyo katika hatari.
Uchambuzi huo unafanywa na shirika la Sweden, Flowminder, kwa kutumia data inayotolewa bila malipo na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom.
Taarifa hizo hukusanywa kwa njia fiche bila watafiti kuingilia taarifa binafsi za watumiaji.
Kisangani, kitovu muhimu cha usafiri, kilitambuliwa mapema kuwa katika hatari kutokana na idadi kubwa ya wasafiri kutoka maeneo yaliyoathiriwa.
WHO iliimarisha maandalizi huko kabla ya visa vya kwanza kugunduliwa.
Hadi sasa, mlipuko huo umeenea katika majimbo sita, huku zaidi ya watu 6,250 wakiambukizwa na 3,039 kufariki tangu mlipuko huo kutangazwa Mei 15. Ugonjwa huo unasababishwa na Bundibugyo, ambayo haina chanjo wala tiba iliyoidhinishwa.
from Taifa Leo https://ift.tt/JHQuscf
via IFTTT
Tags
TRENDING NEWS