Trump aapa kutumia mabavu Democrats wakizidi kumkazia

WASHINGTON, AMERIKA

RAIS Donald Trump ametishia kutuma maajenti wa Idara ya Uhamiaji na Ushuru wa Bidhaa (ICE) kwenye viwanja vya ndege nchini, hii leo iwapo wabunge wa Democrat hawatakubali papo hapo ufadhili wa usalama wa uwanja wa ndege.

“Nitawahamisha maajenti wetu wa ICE waliojawa hekima na wazalendo katika viwanja vya ndege ambapo wataweka usalama ambao haujawahi kamwe kuonekana hapo mbeleni,” Trump aliandika Jumamosi kwenye mtandao wa kijamii wa Truth Social, zaidi ya mwezi mmoja kuelekea hatua ya serikali kufunga kijisehemu cha sekta hiyo.

Wafanyakazi katika idara inayosimamia Usalama wa Usafiri (TSA) wanatazamiwa kukosa mshahara wao kamili kwa mara ya pili Ijumaa kutokana na uamuzi huo wa kufunga huku wabunge wakitofautiana vikali kuhusu ufadhili wa Wizara ya Usalama wa Ndani, taasisi inayojumuisha TSA na ICE.

Maajenti wa ICE hawajapokea mafunzo yanayohusu hasa usalama wa uwanja wa ndege, kiini cha TSA, inayojumuisha waajiriwa 65,000 ikiwemo maafisa 50,000 wa usalama wa uwanja wa ndege.

ICE imetekeleza wajibu muhimu kwenye msako dhidi ya wahamiaji unaoendeshwa na serikali ya Trump, na kuvutia shutuma kutoka kwa wanachama wengi wa Democrats, watetezi wa uhuru wa binadamu na makundi ya kutetea wahamiaji.

Maafisa wa TSA wameomba ruhusa wakisema wanaugua na uhaba wa maajenti wa usalama umetatiza usafiri kwenye viwanja vikubwa vya ndege.

Zaidi ya asilimia 10 ya maafisa wa TSA walituma maombi kwamba wanaugua katika zaidi ya nusu ya siku saba zilizopita, ilisema DHS katika taarifa Jumamosi.

Wafanyakazi zaidi ya 400 wa TSA wameacha kazi tangu mchakato wa kufunga sehemu ya vituo hivyo ulipoanza Februari 14, ilisema DHS, ikieleza kuwa visa vya kujiuzulu na kuomba ruhusu vinatarajiwa “kuongezeka kwa wingi” huku mchakato wa kufunga ukiendelea.

Trump alichapisha kuwa mchakato wa kutuma ICE utaanza leo “iwapo wabunge wa Democrats hawataruhusu Usalama wa Haki na Mwafaka katika viwanja vyetu vya ndege, na kwingineko katika taifa letu.”

Seneta Richard Blumenthal, mwanachama wa Democrat kutoka Connecticut alikosoa pendekezo la Trump akilitaja “tishio lingine linalotolewa kiholela kinyume cha sheria, la kutumia vibaya maajenti wa ICE.”

"Yamkini hafahamu lolote kuhusu vipimo vya ICE, na ninafikiri Amerika itapigwa na butwaa kuona maajenti wa ICE wakizurura viwanja vya ndege, sawia na jinsi wamekuwa wakivunja milango ya makazi,” Blumenthal alieleza wanahabari Washington.

Mwakilishi Bennie Thompson, mwanachama mkuu wa Democrat kwenye Kamati ya Usalama wa Nchi, alisema kupitia taarifa kwamba Trump “anaunda sintofahamu katika viwanja vya ndege kwa sababu za kisiasa” na kuwaweka mawakala wa ICE kwenye vituo vya ukaguzi wa usafiri kutaleta “nyenzo ya udikteta” nchini.

“Donald Trump anahitaji kusimamisha polisi wake wa siri, akubali mageuzi ya ICE yenye urazini, na aturuhusu kuwalipa wafanyakazi wa TSA,” alisema mbunge huyo wa Mississippi.

Elon Musk, ambaye ndiye mkwasi zaidi duniani, Jumamosi alijitolea kulipa mishahara ya TSA “katika kipindi hiki cha mtanziko kuhusu ufadhili ambao umeathiri maisha ya raia wengi wa Amerika.



from Taifa Leo https://ift.tt/AbnD6WN
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post