
MVUTANO mpya wa kisheria umeibuka kuhusu hukumu ya Mahakama Kuu iliyothibitisha kutimuliwa kwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, baada ya baadhi ya walalamishi kudai nakala waliyopewa inatofautiana na ile ambayo majaji walisoma hadharani mahakamani.
Mawakili wa Chama cha Gema Watho Association, ambacho ni mlalamishi wa 41 katika kesi zilizounganishwa kuhusu kutimuliwa kwa Gachagua, wameandikia rasmi Naibu Msajili wa Kitengo cha Katiba na Haki za Kibinadamu wakitaka wapewe hukumu kamili, kumbukumbu za vikao na rekodi za sauti na video za kikao cha Juni 8.
Katika barua yao ya Juni 12, mawakili hao walisema Jaji Eric Ogola aliyesimamia jopo hilo, aliwaambia wahusika kuwa hukumu hiyo ilikuwa ya kurasa 350 na kwamba, majaji watatu waliisoma hadi baada ya saa tatu usiku kabla ya kuitia saini.
Hata hivyo, walidai nakala waliyopewa siku tatu baadaye ilikuwa na kurasa 286 pekee na haikuwa na saini za majaji.
“Ni wazi kuwa kurasa 64 hazipo kwenye hukumu hiyo,” walisema mawakili wa Kiragu Wathuta & Company Advocates, wakiongeza kuwa hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu kupungua kwa kurasa hizo wala kukosekana kwa saini zinazothibitisha uhalali wake.
from Taifa Leo https://ift.tt/yOF9iwf
via IFTTT
Tags
TRENDING NEWS