Dai huenda Ruto akamtema Kindiki kabla ya 2027

NAIBU Rais Profesa Kithure Kindiki huenda asiwe mgombea mwenza wa Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa 2027, Mbunge wa Ndia George Kariuki amedai. Bw Kariuki, ambaye ni mshirika wa karibu wa Rais Ruto, alisema Profesa Kindiki kwa sasa anashikilia wadhifa huo lakini anaweza kubadilishwa kabla ya uchaguzi. Akizungumza na redio ya Kameme, mbunge huyo alipinga madai kwamba Chama cha ODM ndicho kitatoa mgombea mwenza wa Rais Ruto. Alisema nafasi hiyo bado itaenda kwa mtu kutoka eneo la Mlima Kenya, ingawa huenda asiwe Profesa Kindiki. “ODM haitahitajika kutoa mgombea mwenza. Suala hilo litajadiliwa ili kubaini anayefaa zaidi kutoka eneo hili lenye kura nyingi,” akasema. Bw Kariuki pia alisisitiza umuhimu wa wakazi wa Mlima Kenya kubaki na umoja na kukataa mipango ya kugawanya kura za eneo hilo. Majuzi, Bw Kariuki alimvamia Profesa Kindiki akisema ameshindwa kuwatetea wakazi wa Mlima Kenya. Pia aliwakosoa Profesa Kindiki na kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua kwa kushambuliana kisiasa na kugawanya eneo hilo.

from Taifa Leo https://ift.tt/sYI1ZDq
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post