
WASHUKIWA 1,827 wamekamatwa nchini kwa tuhuma za kuhusika katika uhalifu wa magenge kati ya Januari na Agosti mwaka huu, huku 729 wakipatikana na hatia.
Kati ya kesi hizo, 716 bado ziko mahakamani huku serikali ikiongeza msako dhidi ya makundi hayo kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.Idara ya Serikali ya Usalama wa Ndani na Utawala wa Kitaifa, imetambua magenge na makundi 109 ya wahalifu nchini, idadi ambayo imeongezeka kutoka 89 yaliyotangazwa kuwa haramu kupitia Gazeti la Serikali Nambari 10427 la mwaka 2016.Katibu wa Usalama wa Ndani, Dkt Raymond Omollo, alisema serikali haitawalenga watu wanaotekeleza uhalifu pekee, bali pia viongozi, wafadhili na wanaoendesha shughuli za makundi hayo.Trans Nzoia inaongoza kwa idadi ya washukiwa waliokamatwa ikiwa na 491, ikifuatiwa na maeneo mengine yaliyoathiriwa na vitendo vya magenge.
Kwa mujibu wa serikali, magenge hayo yanaweza kutumiwa wakati wa uchaguzi kuvuruga mikutano, kuwatisha wapinzani, kushambulia na kusababisha ghasia.Katibu wa Usalama wa Ndani, Raymond Omollo, alisema serikali haitawalenga watu wanaotekeleza uhalifu pekee, bali pia viongozi, wafadhili na wanaoendesha shughuli za makundi hayo.“Wale wanaoajiri, kufadhili au kuongoza makundi hayo watawajibishwa pamoja na wanaotekeleza ghasia,” alisema.
from Taifa Leo https://ift.tt/Joeqbsi
via IFTTT