Mapema wiki jana Naibu Spika Gladys Boss Shollei pia aliapa kufanya kila awezalo kuhakikisha hoja inapishwa bungeni.
Lakini akiongea Jumamosi katika msururu wa mikutano ya hadhara katika kaunti za Kirinyaga, Embu na Meru, Bw Gachagua alishikilia kuwa alichaguliwa moja kwa moja na wananchi na hivyo wabunge hawana mamlaka ya kumtimua. Alisema alichaguliwa kwa tiketi moja na Rais Ruto na hivyo ikiwa ataondolewa, kiongozi wa taifa pia anafaa kung’atuliwa. “Si mimi na rais tulichaguliwa kwa tiketi moja? Kwa hivyo, wale wanataka kunifuta kazi wajue kuwa nikienda………….hata Rais naye …………” akasema aliposimama kwa muda katika kituo cha kibiashara cha Ngurubani, kaunti ya Kirinyaga akiwa njiani kuelekea Embu. Bw Gachagua aliandamana na wabunge watano pekee akiwemo Mbunge Mwakilishi wa Kirinyaga Njeri Maina na Mbunge wa Juja George Koimburi. Idadi kubwa ya wabunge kutoka eneo la Mlima Kenya wamemtoroka Naibu Rais wakimsuta kwa kuendeleza siasa za kikabila zinazoweza kuleta migawanyiko nchini. Hata hivyo, Bw Gachagua amepata uungwaji mkono kutoka mrengo wa Azimio unaongozwa na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka. Jumapili, kinara huyo wa Azimio aliwaonya wabunge dhidi ya kutia saini hoja ya kumtimua Bw Gachagua akisema mpango huo utatumiwa kuhepa uwajibikaji wa serikalini. “Na wazi kuwa serikali hii imefeli na sasa imeanza mchezo wa kuelekezana lawama. Kenya Kwanza isihusishe Wakenya katika vita vyao vya kindani. “Wabunge nao wasikubali kuhongwa Sh100,000 ili waweke sahihi zao katika hoja hiyo, hatutaki kuelekea mkondo huo. Kabla ya kutia sahihi yako jua kuwa hizo ni mbinu ya kukwepa kushughulikia changamoto kadhaa zinazowakabiliwa Wakenya wakati na kufunika sakata kubwa kama vile uuzaji wa uwanja kwa JKIA kwa kampuni ya Adani,” Bw Musyoka akasema akiwa Kitengela, Kajiado.from Taifa Leo https://ift.tt/ERspVLw
via IFTTT
Tags
TRENDING NEWS