
“Hatutalegeza kamba hadi tushinde taji la KPL. Leo (Jumamosi) nimefurahishwa na jinsi vijana walisuka mechi na kulinda ngome yetu. Nimefurahia jinsi tulifunga mabao yetu mawili kwa sababu yalitokana na ushirikiano murwa.”Mjini Machakos, Police ilipata mabao yake kupitia Mohamed Bajaber aliyefunga mawili naye David Ishura akongeza lingine. Victor Haki alifutia chozi Murang'a Seal. Katika mechi nyingine, KCB waliendelea pia kutia presha timu zilizo juu ya jedwali huku Kelvin Okumu na Francis Kahiro wakiwapa ushindi dhidi ya Ulinzi Stars. Lilikuwa bao la 12 la Kahiro ambaye ameshuhudia ukame wa magoli. Wanajeshi wa Ulinzi waliliwazwa na goli la Joseph Ochieng’ baada ya kumegewa pasi na Boniface Muchiri.
Jedwali
Zikiwa zimesalia mechi 10 kabla ligi ifike tamati maafande wa Kenya Police wanaongoza msimamo wa jedwali na alama 45, Tusker inafuata na alama 44 huku Gor ikiwa nambari tatu na alama 42. Wanabenki wa KCB wamejikusanyia alama 39 baada ya mechi 24 japo pia wamekuwa na matokeo mseto yaliyowaponza baada ya kuongoza KPL kwa wiki kadhaa mkondo wa kwanza. Aidha, Ryan Ogam wa Tusker na Moses Shumah wa Kakamega Homeboyz wanaofukuzia tuzo ya Kiatu cha Dhahabu waliendelea kupata ukame wa magoli wikendi. Ogam anayeongoza orodha ya wafungaji kwa mabao 15 hajacheka na nyavu sasa katika mechi saba mfululizo huku Shumah mwenye magoli 13 akikosa kufunga katika mechi tatu zilizopita za KPL.from Taifa Leo https://ift.tt/1BKqtDe
via IFTTT
Tags
TRENDING NEWS