
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Uganda, Muhoozi Kainerugaba, ametoa onyo kali kwa Uturuki, akitishia kuvunja uhusiano wa kidiplomasia ndani ya siku 30 iwapo malalamishi ambayo hajayaweka wazi hayatashughulikiwa. Kupitia ujumbe mkali aliouchapisha kwenye mtandao wa X mnamo Aprili 11, 2026, Kainerugaba, mwana wa Rais Yoweri Museveni, alisema amechoshwa na kile alichokitaja kuwa kuchelewa kwa muda mrefu kwa upande wa Uturuki kushughulikia masuala yanayowahusu. Kauli hiyo imeibua dalili za mabadiliko makubwa katika uhusiano kati ya nchi hizo mbili. “Tatizo halisi ni Uturuki! Tumewapa muda wajirekebishe lakini hakuna kinachoendelea. Tuko tayari kusitisha kabisa uhusiano wa kidiplomasia ndani ya siku 30 ikiwa hawatashughulikia masuala yetu,” alisema. Mbali na hilo, aliongeza kuwa Uganda inaweza pia kuchukua hatua dhidi ya shughuli za anga za Uturuki, akidokeza uwezekano wa kuwekea vikwazo safari za ndege kati ya nchi hizo mbili iwapo mvutano huo hautatatuliwa. Hata hivyo, bado haijabainika wazi ni nini hasa kinachosababisha mzozo huo. Matumizi ya neno “kujirekebisha” yanaashiria uwezekano wa tofauti za kisiasa, kiusalama au kiuchumi, lakini hakuna taarifa rasmi iliyokuwa imetolewa na serikali ya Uganda au Uturuki kueleza kiini cha tatizo wakati wa kuchapisha habari hii Wachambuzi wa masuala ya kimataifa wanasema hatua ya kuvunja uhusiano wa kidiplomasia ni ya kiwango cha juu sana na mara nyingi hutumiwa kama suluhu ya mwisho pale mazungumzo yanaposhindikana. Hivyo basi, tishio hilo linaweza kuwa na athari kubwa kwa biashara, ushirikiano wa kijeshi na mikataba ya pande mbili kati ya Uganda na Uturuki. Kauli ya Kainerugaba pia inatarajiwa kuzua mjadala mpana katika ukanda wa Afrika Mashariki na kimataifa, huku wadau mbalimbali wakifuatilia kwa karibu maendeleo ya mvutano huo. Muhoozi amekuwa akitoa vitisho kwa nchi kadhaa ikiwemo Kenya jirani ya Uganda upande wa mashariki na hata Ira
from Taifa Leo https://ift.tt/Qq0YUpi
via
IFTTT