
Wakazi wakimiminika eneo ambapo afisa wa GSU aliwapiga risasi na kuwaua mke na mtoto kabla ya kujitoa uhai mjini Mokowe, Lamu Magharibi Jumapili, Mei 11, 2025. Picha|Kalume Kazungu[/caption] “Afisa hakuonyesha dalili yoyote kwamba alikuwa akipitia matatizo. Alitoka kambini kama kawaida kwenda nyumba aliyokodi na mkewe na mtoto ambayo iko nje ya kambi. “Tunashangaa kuarifiwa kwamba ametekeleza mauaji hayo. Maafisa wangu wawe na tabia ya kutafuta ushauri kwa wenzao na hata wakubwa wao wanapopitia changamoto. Kujiua na kuua wengine siyo suluhu,” akasema Bw Changach. Mmoja wa majirani wa wanandoa hao, Bw Mohamed Yusuf, alieleza kushangazwa na tukio hilo. “Tunawafahamu wawili hawa kama wapenzi. Wameishi nasi kwa karibu mwaka mmoja sasa. Mama ni mwalimu ilhali mume ni polisi wa GSU. Hatujawahi kusikia wakizozana. Mauaji yametupata kwa mshangao mkuu,” akasesma Bw Yusuf. Mtaalamu wa Masuala ya Kisaikolojia na Ushauri Nasaha anayehudumia Hospitali ya Mpeketoni, Bw Andrew Masama, aliwasihi wanandoa na wapenzi kuwa wazi ili kuepuka migogoro nyumbani. Alisema maafisa wa polisi mara nyingi tayari hupitia changamoto tele na msongo wa mawazo karibu kila siku kazini. “Ombi langu kwa wanandoa na hata wapenzi ni kwamba tuweni na uwazi ili kuepuka migogoro na mauaji. Pia tutafute ushauri nasaha tunapokumbwa na changamoto za maisha, ziwe za kikazi au kijamii,” akasema Bw Masama.from Taifa Leo https://ift.tt/kbqFKTB
via IFTTT
Tags
TRENDING NEWS