Muhoozi atoa amri majenerali wawili wakamatwe kwa tuhuma za ufisadi

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi nchini Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba alitoa amri ya kukamatwa kwa Meja jenerali Don William Nabasa na Brigedia Johnson Namanya Abaho kutokana na tuhuma za ufisadi. Amri hiyo iliyoelekezwa kwa Inspekta Jenerali wa vikosi vya ulinzi Lt Jenerali Sam Okiding ilitekelezwa mara moja. Jenerali Okoding aliwakamata wawili hao na kuwazuilia katika kituo cha Mbuya, kisha wakahojiwa kwa kina kabla ya kuhamishwa na kupelekwa katika kituo kingine. Awali, wawili hao walizuiliwa katika kituo cha Kasenyi chenye Vikosi Maalum kwenye barabara ya Entebbe kabla ya kuhamishwa. "Maafisa hao wapo chini ya ulinzi huku wakisubiri amri nyingine ya kuwazuia hapa ama kuwahamisha hadi kituo cha wanajeshi cha Makindye,” alisema afisa mmoja. Kwa sasa simu za majenerali hao zimezima.  

from Taifa Leo https://ift.tt/DbovWGP
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post