Saini ya Trump kutumika kwenye noti ya Amerika kuanzia Juni

SARAFU ya Amerika inatarajiwa kubadilika huku saini ya Rais Donald Trump ikitarajiwa kuanza kutumika kuanzia Juni hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa rais aliye madarakani kutia saini kwenye fedha za nchi hiyo.

Idara ya Hazina ilisema kuwa noti hizo mpya zinatarajiwa kuadhimisha miaka 250 ya uhuru wa Amerika, pia itakuwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 165, kuwacha kutumia saini ya mweka hazina ambaye huripoti kwa waziri wa Hazina.

Noti za kwanza za dola 100 (Sh12,990) zenye sahihi ya Trump na Katibu wa Hazina Scott Besset zitachapisha mwezi Juni, ikifuatiwa na noti zingine katika miezi inayofuatwa.

Noti hizo mpya zinaweza kuchukua wiki kadhaa kuanza kusambazwa kupitia mabenki.

Kwa sasa hazina inaendelea kuchapisha noti zenye saini za aliyekuwa Rais Joe Biden kupitia katibu wake wa Hazina Janet Yellen, pamoja na mweka Hazina wa zamani Lynn Malerba.
Noti za fedha duniani mara nyingi huonyesha saini ya gavana wa benki kuu, waziri wa fedha au afisa mwingine anayehusika na uchapishaji na utoaji wa fedha.
Saini ya Trump itachukua nafasi ya ile ya Mweka Hazina wa Amerika ambayo imekuwa ikitumika kwenye sarafu za Amerika tangu mwaka 1861.
Saini ya Waziri wa Hazina iliongezwa takribani karne moja iliyopita na itaendelea kuwepo pamoja na ya Trump.



from Taifa Leo https://ift.tt/cMdjapY
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post