Afueni bei ya dizeli ikipunguzwa kwa Sh5

WAKENYA wamepata afueni baada ya Serikali kupunguza bei ya dizeli kwa Sh5 kwa lita, hatua inayotarajiwa kupunguza gharama za usafiri na bidhaa.
Mamlaka ya Kudhibiti Kawi na Petroli (EPRA) imesema bei hiyo mpya itaanza kutumika kuanzia Agosti 15 hadi Septemba 14, 2026.
Hata hivyo, bei ya Super Petrol na mafuta ya taa haitabadilika kwa kipindi cha mwezi mmoja ujao.
Serikali imetenga Sh938 milioni katika hatua ya kudhibiti bei, huku ikilenga kuwalinda wananchi dhidi ya mabadiliko ya bei katika soko la kimataifa.
Katika bei zilizokuwa zikitumika hadi Agosti 14, lita moja ya Super Petrol iliuzwa kwa Sh214.03 jijini Nairobi, huku dizeli ikiuzwa kwa Sh222.86 na mafuta ya taa kwa Sh191.38.
EPRA ilisema bei hizo zinajumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), pamoja na ushuru na ada nyingine.
Kupungua kwa bei ya dizeli kunatarajiwa kuwapa nafuu wenye magari, wafanyabiashara na sekta zinazotegemea uchukuzi.


from Taifa Leo https://ift.tt/TkUdIXl
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post