
MIAMBA Arsenal wameibuka mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya washindani wao wakuu, Manchester City kulazimishiwa sare na vidume FC Bournemouth.
Baada ya miaka 22 ya ukame, kibaridi na kejeli kutoka kwa watani wao,
The Gunners hatimaye wamefaulu kujinasia taji hilo la msimu wa 2025-26 Jumanne usiku pale vigogo wa muda mrefu Man City walipokosa kujipatia ushindi dhidi ya
The Cherries ambao nao walikuwa wanafukuzia angalau alama moja ili wafaulu kushiriki kombe la Uefa Conference Cup msimu ujao.
Man City walikuwa nyuma ya Arsenal kwa alama tano wakienda ugani Vitality baada ya vijana wa kocha Mikel Arteta kutekeleza jukumu lao kwa kunyuka Burnley Jumatatu.
Sare ya 1-1 baina ya City na Bournemouth inamaanisha kwamba wakiwa na alama 78 dhidi ya 82 za Arsenal jedwalini, alama za juu zaidi wanazoweza kupata ni 81 kwenye mechi ya funga msimu hata kama Arsenal watapoteza dhidi ya Crystal Palace Jumapili.
from Taifa Leo https://ift.tt/ZOUM2dI
via
IFTTT