Wapigakura wapya na maana yake kwa 2027

Zaidi ya Wakenya milioni 2.34 walijisajili kuwa wapigakura ndani ya mwezi mmoja tu, ongezeko kubwa linaloweza kubadili kwa kiasi kikubwa mwelekeo wa siasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027.

Kulingana na takwimu za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Jiji la Nairobi liliongoza kwa kusajili wapigakura wapya 276,886.

Kaunti ya Kiambu ilifuata kwa wapigakura 128,859, ikifuatiwa na Nakuru (102,207), Kakamega (93,858), Machakos (84,198) na Bungoma (73,599). Kaunti nyingine zilizorekodi ongezeko kubwa ni Meru (67,651), Kilifi (65,572), Kisii (65,152) na Uasin Gishu (64,774). Kitui ilisajili 61,839 huku Turkana ikiwa na 58,428 na Kajiado 55,013.

Katika Bonde la Ufa, pamoja na Uasin Gishu, Nandi ilisajili wapigakura 52,630, Kericho (52,290), Narok (46,794) na Bomet (44,637). Pwani pia ilichangia kwa kiasi kikubwa huku Mombasa ikisajili 51,286 na Kwale 29,375.

Nyanza nayo ilionyesha ushindani mkali, Homa Bay ikiongoza kwa 53,553, ikifuatiwa na Migori (46,620), Kisumu (45,280) na Siaya (44,078).

Maeneo ya Mlima Kenya pia yalikuwa na ongezeko, Murang’a (49,791), Nyeri (46,552), Kirinyaga (36,617) na Embu (22,999).

Kaskazini mwa Kenya, ambako kwa kawaida usajili huwa mdogo, pia kulirekodi mafanikio, huku Garissa ikisajili 24,575, Wajir (21,171), Mandera (18,214), Marsabit (23,267) na Isiolo (10,632).

“Ingawa idadi ni ndogo ikilinganishwa na mijini, kura hizi zinaweza kuwa muhimu katika ushindani mkali wa kitaifa,” alisema mchambuzi wa siasa Dismas Mokua.

IEBC ilisema zoezi hii ilikuwa hatua muhimu, ikiwa na jumla ya wapigakura wapya 2,345,476 kati ya Machi 30 na Aprili 28, 2026.

Wachambuzi sasa wanasema kuwa ongezeko hili linaashiria kuanza mapema kwa siasa za 2027, huku vyama vikilenga kuimarisha ngome zao na kuvutia maeneo ya ushindani.



from Taifa Leo https://ift.tt/sR4C6Pu
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post