Ruto ana kibarua kigumu kuvumisha Tutam Wakenya wakikabiliwa na gharama ya juu ya maisha

UCHAGUZI Mkuu wa 2027 umeibua hali ya kipekee katika siasa za Kenya.
Rais William Ruto anaingia katika kipindi cha mwisho cha muhula wake wa kwanza akiwa amepoteza sehemu kubwa ya uungwaji mkono wa wananchi, lakini wapinzani wake bado hawajakubaliana kuhusu nani atapeperusha bendera ya muungano wao.
Huku gharama ya maisha, madai ya ufisadi na ukosefu wa ajira vikiendelea kuwakera wananchi, viongozi wa upinzani wameendelea kushindwa kupata mwafaka kuhusu mgombea mmoja wa urais.
Badala yake, wamejikita katika mijadala ya ndani kuhusu vigezo vya kumchagua mgombea.Kwa sasa, upinzani umejigawa katika makundi mawili yasiyosajiliwa rasmi.
Kundi la United Alternative Government linawajumuisha Kalonzo Musyoka, Rigathi Gachagua, Martha Karua, Eugene Wamalwa na George Natembeya.
Upande mwingine kuna Linda Mwananchi ambako Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna ametajwa kama mmoja wa wanaoweza kuwania urais.
Mipango ya kufanya kikao maalum cha kuamua mgombea wa pamoja imeahirishwa mara kadhaa.
Viongozi hao wamependekeza vigezo tisa vya kuchagua mgombea wao, ikiwemo umaarufu, tafiti za kisayansi.


from Taifa Leo https://ift.tt/Veyw68Y
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post